Omari Omari arejea Mashujaa kwa Mkopo

Kiungo mshambuliaji, Omari Omari amejiunga kwa mkopo na Mashujaa FC wa mwaka mmoja kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano 2025/2026.

Omari alijiunga nasi msimu uliopita akitokea Mashujaa kwa mkataba wa miaka mitatu na sasa amerejea kwa mkopo kwa ‘Wanajeshi hao wa Mpakani’.

Omari ni miongoni mwa wachezaji vijana wenye vipaji vikubwa ambao wanategemewa kujakuwa msaada mkubwa kwa Taifa katika siku za baadae ingawa msimu uliopita hakupata nafasi kubwa ya kucheza.

Menejimeti ya klabu na mchezaji wamekubaliana nyota huyo kurejea Mashujaa kwa manufaa ya pande zote.

Simba inamtakia heri Omari katika kipindi chote atakachokuwa kwa mkopo kwenye timu ya Mashujaa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER