Sita waitwa Stars kujiandaa na CHAN

Nyota wetu sita wamejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Taifa Stars itaingia kambini Julai 7 kujiandaa na michuano hiyo ambayo Tanzania ni miongoni mwa nchi mwenyeji.

Mlinda mlango Aishi Manula amerejeshwa kwenye kikosi cha stars baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kufuatia majeraha yaliyokuwa yanamsumbua.

Nyota wengine walioitwa ni walinzi Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ na Abdulrazack Hamza.

Wengine ni kiungo Yusuph Kagoma na kiungo mshambuliaji Kibu Denis.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER