Tumepoteza Dabi ya Kariakoo

Mchezo wetu wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-0.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikisomana zikiwa zimechukua tahadhari kubwa kuhakikisha haifanyi makosa yatakayowafanya kuruhusu bao.

Dakika 15 za mwanzo tulifika zaidi langoni mwa Yanga kabla na wao kufika kwetu kwenye 15 za pili ingawa pamoja na mashambulizi lakini hakuna bao lililopatikana.

Pacome Zouzoua aliipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 65 kwa mkwaju wa penati baada ya mlinda mlango Moussa Camara kumfanyia madhambi ndani ya 18.

Clement Mzize aliwapatia Yanga bao la pili dakika ya 85 akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Zouzoua.

Mchezo huu umekamilisha rasmi msimu wa ligi 2024/25 ingawa tumekosa taji lakini tumepata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

X1: Diara, Mwenda, Boka, Bacca, Job, Aucho, Nzengeli (Nzengeli 70′), Abuya, Dube (Mzize 45′), Mudathir (Ikangalombo 90′), Pacome

Waliionyeshwa kadi: Pacome 21′ Mzize 85′ Boka 90+1

X1: Camara, Kapombe (Nouma 79′), Zimbwe Jr, Chamou (Awesu 66′) Che Malone, Kagoma (Hamza 66′), Mutale (Kibu 45′) Ngoma, Mukwala (Ateba 54′) Ahoua, Mpanzu

Waliionyeshwa kadi: Zimbwe Jr’

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER