Baada ya kurejea salama jijini Dar es Salaam kutoka Afrika Kusini, kikosi kimepewa mapumziko ya siku moja ambapo kesho kitarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs.
Kikosi kimewasili saa sita mchana ambapo wachezaji wamepewa muda wa kukutana familia zao kabla ya kuanza mawindo dhidi ya Kaizer kesho.
Tunaingia kwenye maandalizi ya mchezo huo tukijua tunahitaji kufanya kazi kubwa ya kugeuza matokeo mabaya ya mabao 4-0 tuliyopata ili kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano hii.
Mchezo wa marudiano utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jumamosi Mei 22 saa nane mchana.