Timu yetu ya Simba Queens imetawazwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) 2020/21 baada ya kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Baobab Queens mchezo uliopigwa Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa dakika ya mwisho ya 94 na kiungo mshambuliaji Asha Djafar na kufanikisha kutwaa taji hilo.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Simba Queens kutwaa ubingwa huo, wakifanikiwa kufikisha pointi 54 alama moja juu ya Yanga Princess iliyomaliza nafasi ya pili.
Hatua hiyo inaipa nafasi Simba Queens kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika upande wa Wanawake kuanzia msimu ujao wa 2021/22.
Simba Queens imemaliza michuano hiyo ikishinda mechi 17 kati ya 20 na kutoka sare mitatu ikiwa haijapoteza mchezo wowote.
Hii inamaanisha Simba Queens imetwaa ubingwa bila kufungwa ‘unbeaten’.
One Response
Hongera Simba Queens