Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Mkuu Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji wa sita ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi iliyopita dhidi ya Kengold.
Kocha Fadlu amewaanzisha David Kameta ‘Duchu’ Valentine Nouma, Fabrice Ngoma, Ladaki Chasambi, Steven Mukwala na Awesu Awesu wakichukua nafasi za Shomari Kapombe Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ Yusuph Kagoma, Kibu Denis, Leonel Ateba na Elie Mpanzu.
Kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (26), David Kameta (3), Valentine Nouma (29), Che Malone (20), Fabrice Ngoma (6), Ladaki Chasambi (36), Debora Fernandes (17), Steven Mukwala (11), Jean Charles Ahoua (10), Awesu Awesu (23).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Augustine Okajepha (25), Joshua Mutale (7), Leonel Ateba (13), Kibu Denis (38), Elie Mpanzu (34), Valentine Mashaka (27), Bashir Salum (59)