Alichosema Kocha Matola kuelekea mchezo dhidi ya Kengold

Kocha Msaidizi, Seleman Matola ameweka wazi kuwa pamoja na Kengold kuwa wameshuka daraja lakini hatutawadharau kwakuwa tunahitaji kupata alama tatu muhimu ugenini.

 

Matola amesema malengo yetu ni kutwaa ubingwa na ili kufanikisha hilo tunahitaji kushinda mechi zetu zote tatu zilizobaki tukianza kesho dhidi ya Kengold.

Matola ameongeza kuwa tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Kengold na tumejiandaa kuhakikisha tunapata alama zote tatu.

Akizungumzia hali ya kikosi, Matola amesema wachezaji wote waliopo kikosini wapo kwenye hali nzuri na wameshiriki kikamilifu mazoezi ya mwisho na hakuna aliyepata majeraha ambayo yatamfanya kuukosa mchezo.

“Sisi tuna malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu, na ili kufanikisha hilo tunahitaji kushinda mechi zote tatu zilizobaki. Tunajua Kengold wameshuka daraja lakini tunafahamu watatupa upinzani mkubwa ingawa tumejipanga kuwakabili,” amesema Matola.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu amesema wapo kamili kuhakikisha malengo ya alama tatu ugenini yanafikiwa.

“Kila mchezaji anafahamu mchezo utakuwa mgumu na malengo yetu ni kupata pointi tatu kwahiyo yoyote atakayepata nafasi atakuwa tayari kupambana muda wote ili kupata ushindi ugenini,” amesema Awesu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER