Tumeshindwa kutinga fainali ya CRDB Federation

Mchezo wetu wa nusu fainali ya CRDB Federation Cup uliopigwa uwanja wa Tanzanite Kwaraa umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 3-1 na kushindwa kutinga fainali.

Jonathan Sowah aliwapatia Singida bao la kwanza dakika ya 16 kwa shuti kali la chini chini akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea kutoka kwa Frank Assinki.

Mlinda mlango Moussa Camara alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kugongana na Sowah nafasi yake ikachukuliwa na Ally Salim dakika ya 28.

Emmanuel Keyekeh aliipatia Singida bao la pili dakika ya 34 kwa mguu wa kushoto baada ya makosa yaliyofanywa na mlinda mlango Ally Salim.

Keyekeh aliipatia Singida bao la tatu kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja dakika ya 48 baada ya mchezaji mmoja kufanyiwa madhambi nje ya 18.

Jean Charles Ahoua alitupatia bao la kwanza dakika ya 68 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja nje ya 18 baada ya Mutale kufanyiwa madhambi.

X1: Camara (Salim 28′), Duchu, Nouma (Zimbwe Jr 59′), Hamza, Che Malone (Karaboue 45′), Kagoma (Fernandez 50′), Kibu (Mpanzu 50′), Ngoma, Mukwala, Ahoua, Mutale

Waliionyeshwa kadi: Kagoma 34′ Mpanzu 54′ Chamou 64′ Ngoma 76′

X1: Obasogie, Koffi, Gadiel, Assinki, Kennedy, Damaro, Edmund (Tchekei 74′), Chukwu (Tra Bi 74′) Sowah (Rupia 60′), Keyekeh, Bada

Waliionyeshwa kadi: Damaro 4′ Assinki 31′ Chukwu 45+4,

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER