Matola: Tupo tayari kuwakabili Singida Kesho

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema kikosi chetu kipo tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Black Stars utakaopigwa katika uwanja wa KMC Complex saa 10 jioni.

Matola amesema baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye ligi na mipango yetu kuhakikisha tunapata matokeo chanya katika mchezo wa kesho.

Matola ameweka bayana kuwa Singida ni timu imara na tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini hata hivyo tumejipanga vizuri kuhakikisha tunachukua alama zote tatu nyumbani.

“Tunafahamu tuenda kucheza mechi ngumu kesho, Singida Black Stars ni timu bora na ina kikosi imara na hizi ni mechi za mwisho za kuamua ubingwa tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi,” amesema Matola.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ amesema pamoja na ubora walionao Singida lakini tupo tayari kupambana mpaka mwisho ili kupata alama tatu.

“Sisi kama wachezaji tumejiandaa kuhakikisha tunashinda nakuchukua alama tatu, kucheza mechi mbili ndani ya siku nne haitakuwa changamoto ya kushindwa kupata ushindi kesho tupo tayari na tumejipanga,” amesema ‘Duchu’.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER