Droo ya hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) imetoka wmbapo kikosi chetu kimepangwa kucheza na Dodoma Jiji.
Katika mchezo huo utakaochezwa Mei…. Katika Uwanja wa… Simba itakuwa nyumbani.
Simba tukiwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, tunakutana na Dodoma kwa mara ya kwanza katika michuano hii huku ikiwa mara ya tatu katika msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom tukiwafunga mechi zote mbili.
Katika mchezo wa mwisho tuliokutana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Aprili 27 tuliwafunga mabao 3-1 ambapo mawili yalifungwa na Chris Mugalu na Luis Miquissone.
Mechi za hatua ya robo fainali zitachezwa kati ya Mei 25, 26 na 27 ambapo mshindi wa mchezo baina yetu atakutana na mshindi kati ya Rhino Rangers dhidi ya Azam FC katika hatua ya Nusu Fainali.