Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Mkuu Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji watano ukilinganisha na kikosi kilichoanza mechi ya mwisho ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini.
Fadlu amewaanzisha David Kameta, Valentine Nouma, Edwin Balua, Debora Fernandes na Leonel Ateba ambao wamechukua nafasi za Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Fabrice Ngoma, Kibu Denis na Steven Mukwala.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (26), David Kameta (3), Valentin Nouma (28), Karaboue Chamou (2), Abdulrazak Hamza (14), Yusuph Kagoma (21), Edwin Balua (37), Debora Fernandes (17), Leonel Ateba (13), Awesu Awesu (23), Elie Mpanzu (34).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Shomari Kapombe(12), Mohamed Hussein (15), Che Malone Fondoh (20), Augustine Okejepha (25), Joshua Mutale (7), Steven Mukwala (11), Kibu Denis (38), Alexander Erasto (42), Adolf Hamis (50).