Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kwa takribani miaka sita Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Rais wa Klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ amekuwa na ndoto ya kuiona Simba ikitwaa ubingwa wa CAF na sasa maono yake ya natarajiwa kufikia.
Ahmed amesema mara zote Mo amekuwa akisisitiza timu kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika na sasa tumefika fainali na tunapambana kutwaa taji la Kombe la Shirikisho.
Ahmed amesema katika hatua tuliyofikia Uongozi wote wa klabu haukulala kuhakikisha malengo haya yanatimia huku tukiwa hatua chache kabla ya kuchukua ubingwa.
Ahmed ameongeza kuwa wapinzani wetu RS Berkane ni timu nzuri na tunaiheshimu lakini ipo kwenye daraja sawa na letu hivyo tunaweza kuwafunga na kutwaa taji.
“Mara zote Mo Dewji amekuwa akisisitiza kuwa anataka kuiona timu ikichukua ubingwa wa Afrika na msimu huu maono yake yanakwenda kutimia Insha Allah.
“Mara ya mwisho kucheza fainali ya michuano hii ilikuwa mwaka 1993 lakini hatukuweza kutwaa taji ila safari hii tuna nafasi ya kuchukua ubingwa na hili litawezekana pasi na shaka yoyote,” amesema Ahmed.