Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema kikosi kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakaopigwa Jumapili saa 10 jioni katika Uwanja wa Moses Mabhida.
Ahmed amesema hali ya hewa ni baridi lakini sio kali sana ambayo itawafanya wachezaji washindwe kufanya vizuri huku matumaini makubwa ya kupata matokeo chanya yakiwa ni makubwa.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Ahmed amesema hata Stellenbosch sio wenyeji katika mji wa Durban hivyo tutakuwa na faida kubwa.