Kikosi kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Amaan Zanzibar kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakaopigwa Jumapili Aprili 20, saa 10 jioni.
Kikosi kimewasili jana hapa Zanzibar tayari kwa mchezo huo ambao malengo yetu ni kuhakikisha tunapata ushindi mzuri nyumbani ili kujiweka kwenye hali nzuri katika mechi ya marudiano ugenini.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na morali zao zipo juu na wanaonekana wapo tayari ajili ya kuipambania timu kufikia malengo tuliyojiwekea.
Kikosi kitaendelea na programu ya mazoezi kesho na keshokutwa kabla ya kushuka dimbani siku ya Jumapili.