Ahmed: Wazanzibar ipelekeni Simba Fainali ya Shirikisho Afrika

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amewaomba mashabiki hasa kutoka Visiwani Zanzibar kuhakikisha wanapambana na kuiwezesha timu kutinga fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Ahmed amesema ni zamu ya watu kutoka Zanzibar kuweka historia ya kuipeleka timu kutinga fainali ya michuano hii ambayo safari tumedhamiria kutwaa taji lenyewe.

“Niwaombe watu wa Zanzibar na hasa mashabiki wa Simba wafanye kila kinahowezekana kuipeleka Simba fainali. Nilisema kila kizazi na historia yake, hii imekuja wakati muafaka na sisi kuandika historia ya kuipeleka Simba fainali. Tufanye kila kinachowezekana Mnyama kwenda fainali,” amesema Ahmed.

Ahmed ameongeza kuwa “wapinzani wetu Stellenbosch sio timu dhaifu, hadi inafika hatua hii inaonyesha ni timu ambayo imejiandaa. Wanasimba wote tulijiandaa kucheza na Zamalek lakini Stellenbosch akammaliza pale pale nyumbani kwake, hajamtoa Zamalek kwa bahati mbaya.”

Ahmed amewataka Wanasimba kutoidharau timu hiyo kutokana nakuwa timu changa na kuacha kuingia na matokeo uwanjani bali kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anaiwezesha timu kutinga fainali.

“Ni kweli Stellenbosch ni timu ngeni lakini ina wachezaji wenye ubora mkubwa na wana kocha mkubwa. Tuna kazi kubwa kwelikweli kuhakikisha tunamthibiti, tunamfunga ili tukienda kwenye mechi ya ugenini ni iyenaiyena Mnyama hadi fainali,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER