Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu ameweka wazi kuwa pamoja na kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika bado hatuna presha wala hofu ya kutinga nusu fainali kwa kuitoa Al Masry siku ya Jumatano.
Mangungu amesema katika Uwanja wa Benjamin Mkapa haujawahi kushindwa jambo na kupitia umoja na mshikamano wetu hakuna namna Al Masry wataweza kuepuka kipigo kutoka kwetu kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani.
Tazama video hii hadi mwisho Mangungu pia amefunguka ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka Serikalini katika kipindi hiki cha maandalizi.