Tumetoa Msaada Kituo cha Baba Oreste Bunju A

Simba kwa kushirikiana na Taasisi ya Mo Dewji Foundation tumetoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwenye Kituo cha kulelea watoto yatima na wenye uhitaji Maalum cha Baba Oreste kilichopo Bunju A ikiwa ni sehemu ya kurejesha kwa Jamii.

Huu ni utaratibu ambao tumejiwekea wa kurejesha kwa jamii kila tunapoelekea kwenye mechi zetu za nyumbani za Kimataifa lengo likiwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu aweze kutusaidia kufikia malengo yetu.

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema mara zote Simba tumekuwa tukiwathamini wenye uhitaji ambao watu wengi wamekuwa wagumu kuwafikia ambapo mahitaji yao ni makubwa lakini jamii imewasahau.

“Klabu ya Simba inafahamu mahitaji makubwa mnayohitaji. Baba Oreste tayari ametimiza wajibu wake wa kujenga Kituo hiki kilichobaki ni sisi jamii kukiendeleza ndio maana kwa kushirikiana na Mo Dewji Foundation tupo hapa kutoa msaada ikiwa ni maombi kwa Mungu ili kuweza kufanikiwa kwenye mchezo wetu wa Jumatano dhidi ya Al Masry,” amesema Ahmed.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Baba Oreste, Mauricio Obino amesema Kituo hicho kilianzishwa mwaka 2007 kwa dhumuni la kuwasaidia watoto yatima na wenye uhitaji na leo imekuwa furaha kubwa kwao kupokea msaada kutoka Klabu ya Simba na Mo Dewji Foundation.

“Tunawashukuru Simba kwa kuona umuhimu wa kutoa msaada huu, tumefurahi mmetukumbuka nasi tutafanya maombi kwa Mungu ili aweze kuwasaidia kufikia malengo yenu ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa Jumatano,” amesema Bwana Mauricio.

Nae Mkuu wa Mawasiliano na Ushirikiano kutoka Mo Dewji Foundation, Emmyrose Rugumamu amesema lengo la Taasisi hiyo ni kuisaidia jamii katika nyanja mbalimbali bila kujali dini, rangi, kabila ndio maana leo wamefika Baba Oreste kutoa msaada.

“Lengo la Mo Dewji Foundation ni kuisaidia jamii, tupo hapa kutoa msaada kwa watoto wetu hawa na kuimarisha umoja na Ushirikiano,” amesema Emmyrose.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER