Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa mchezo wetu marudiano wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao umepangwa kupigwa Aprili 9, 2025 utafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Ahmed amewatoa hofu Wanasimba kutokana na Uwanja wa Benjamin Mkapa kufungiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa ajili ya kupisha maboresho lakini kwa sasa ni zaidi ya asilimia 100 mtanange huo utapigwa kwenye dimba hilo.
Ahmed amesema majibu ya maboresho ya uwanja huo bado hayajatolewa rasmi na CAF lakini kwa mujibu wa maafisa kutoka Shirikisho hilo ambao wiki iliyopita walikuja kuukagua wamesema sehemu kubwa imefanyiwa marekebisho na hadi kufikia siku ya mchezo yatakuwa yamekamilika.
“Niwatoe hofu Wanasimba kuwa mchezo wetu dhidi ya Al Masry utapigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa na maandalizi yetu yanafanyika huku tukiwa tunajua mechi itapigwa kwa Mkapa,” amesema Ahmed.
Ahmed ameongeza kuwa kutokana na ukubwa na umuhimu wa mchezo huo tayari viingilio vimetangazwa na tiketi zimeanza kuuzwa.
Viingilio vya mchezo huo ni kama ifuatavyo:
VIP A Sh.40,000
VIP B Sh.30,000
VIP C Sh.15,000
Machungwa 10,000
Mzunguko Sh.5000
Platinumz Sh.150,000
Tanzanite Sh.250,000