Kiungo mshambuliaji, Luis Miquissone amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa Ligi Kuu wa mwezi Machi.
Tuzo hiyo alikakabidhiwa jana Jumanne Aprili 27 kabla ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.
Miquissone amekabidhiwa tuzo pamoja na hundi ya Sh 1,000,000 kutoka kwa Wadhamini wa Ligi Kuu Kampuni ya Vodacom kama sehemu ya zawadi hiyo.
Miquissone ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na amedhihirisha hilo kuanzia kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hadi mechi za Ligi Kuu.
Katika mchezo wa jana ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 3-1 Miquissone alitupia bao moja na kuendelea kudhihirisha kuwa yupo kwenye kiwango bora.