Miquissone, Wawa warejea kuivaa Dodoma Jiji

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema kiungo mshambuliaji Luis Miquissone na mlinzi wa kati Pascal Wawa, watakuwepo kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Nyota hao walikosekana katika mchezo uliopita dhidi ya Gwambina FC kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano ambapo sasa wamerejea tayari kwa mechi ya kesho.

Matola amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na anatarajia mchezo utakuwa mgumu lakini kikosi kimejiandaa kushinda ili kuendelea kusogolea lengo letu la kutetea ubingwa msimu huu.

Nahodha huyo wa zamani wa Simba amesema kuelekea mchezo wa kesho tutakosa huduma ya kiungo Taddeo Lwanga ambaye yupo nchini kwao Uganda kuhani msiba wa dada yake.

“Tunawaheshimu Dodoma ni timu nzuri na tunafahamu mechi itakuwa ngumu lakini tumejiandaa kushinda ili kutetea ubingwa wetu,” amesema Matola.

Kwa upande wake nahodha msaidizi Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema baada ya kurudi uwanja wa nyumbani tutahakikisha tunapata ushindi ili kuwafurahisha mashabiki wetu pamoja na kuendelea kubaki kileleni ili kufanikisha lengo la kutetea ubingwa.

“Tuko nyumbani tunataka kuhakikisha Tunaondoka na alama tatu muhimu makocha wametuelekeza tunachotakiwa kukifanya kilichobaki ni sisi kutimiza majukumu yetu uwanjani,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Habari wanasimba wenzangu, kwanza Hongera sana. Timu inazidi kuwa imara na tishio kila siku hapa nchini na hata mashindano makubwa Kama CAF CHAMPIONS LEAGUE.

    Maoni yangu siku ya Leo yanalenga kuendelea kuboresha tu timu yetu tuipendayo. Napendekeza tupate INDIVIDUAL PERFORMANCE ANALYST. Huyu atakuwa msaada mkubwa sana kwa CULVIN. Kuboresha kiwango cha mchezaji mmoja mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER