Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kuelekea mchezo huo kocha Mkuu Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ukilinganisha na kikosi kilichocheza dhidi ya Namungo FC.
Fadlu amemuanzisha Kibu Denis akichukua nafasi ya Ladaki Chasambi ambaye yupo benchi.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Abdulrazack Hamza (14), Che Fondoh Malone (20), Yusuph Kagoma (21), Kibu Denis (38), Fabrice Ngoma (6), Leonel Ateba (13), Jean Charles Ahoua (10), Elie Mpanzu (34).
Wachezaji wa Akiba
Ally Salim (1), David Kameta (3), Valentine Nouma (29), Karaboue Chamou (2), Debora Fernandes (17), Ladaki Chasambi (36), Awesu Awesu (23), Steven Mukwala (11), Valentino Mashaka (27). Alexander Erasto (42).