Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema kwa ukubwa wa kikosi chetu hatuna shaka ya kupangwa na timu yoyote katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Ahmed akiwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Klabu, Zubeda Sakuru ni miongoni mwa waalikwa kwenye sherehe ya upangaji wa droo ya michuano hiyo ambayo itafanyika Doha, Qatar leo saa 11 kwa saa za Tanzania.
Ahmed amesema Simba ni timu kubwa na tupo tayari kupangwa na timu yoyote kati ya Stellenbosch ya Afrika Kusini, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Al Masry ya Misri.
“Sisi kama Simba tupo tayari kupangwa na yoyote, ukiangalia timu zote tatu ambazo tunatarajia kupangwa nazo tumezizidi uzoefu wa mashindano pamoja na ukubwa.”
“Lakini kwa kuangalia jografia ya nchi yetu kama tungepewa nafasi ya kuchagua mpinzani, tungemchangua Stellenbosch kwakuwa Afrika Kusini ni karibu na tunaweza kusafiri na mashabiki wetu na pia kule kule tuna Matawi hivyo hatutakuwa na ugeni,” amesema Ahmed.