Kocha Msaidizi, Suleiman Matola amesema Mwadui walicheza kwa nidhamu kubwa dhidi yetu hatua iliyosababisha kupata ushindi mwembamba wa bao moja.
Amesema Mwadui walifahamu ubora wetu hivyo walicheza kwa nidhamu walikaba wote na kufanya mashambulizi ya kushtukiza hivyo kuubana uwanja.
Hata hivyo Matola ameongeza kuwa Mwadui walikuwa bora na walijitahidi kutuhimili ingawa tuliwazidi uzoefu na kufanikiwa kupata ushindi.
“Mwadui walicheza kwa nidhamu, walituheshimu sana walikaba wote na kushambulia ila kikubwa ni pointi tatu tunajipanga kwa mchezo ujao,” amesema Matola.
Baada ya mechi ya leo tunajiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Gwambina utakaopigwa uwanja wa Gwambina uliopo Misungwi jijini Mwanza Aprili 21, mwaka huu.
One Response
Tupambane ili tutee ubingwa wetu