Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate FC uliopigwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.
Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini sisi tulifika zaidi langoni kwa Fountain Gate.
Dakika 15 kabla ya kuelekea mapumziko tuliongeza mashambulizi langoni mwa Fountain Gate lakini kikwazo kilikuwa mlinda mlango John Noble.
Leonel Ateba alitupatia bao la kwanza dakika ya 57 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ladaki Chasambi.
Fountain Gate walisawazisha bao hilo dakika ya 75 baada ya Chasambi kujifunga wakati aliporudisha mpira mrefu uliomshinda mlinda mlango Moussa Camara.
Mlinda mlango John Noble alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya pili ya nyongeza baada ya kupoteza muda.
X1: Noble, Kadikilo, Kihimbwa (Hasheem 64′), Edgar (Razaq 64′) Kulandana (Ndurie 64′), Mtambi, Sadik, Joram, Shiga, Pandu, Mudrik
Walioonyeshwa kadi: Joram 35′ Kadikilo 40′ (Noble 45′ 90+3′) Edgar 63′
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 85′) Che Malone, Hamza, Kagoma, Chasambi (Mukwala 80′), Ngoma (Mutale 80′), Ateba, Ahoua (Fernandez 71′), Mpanzu
Walioonyeshwa kadi: Chasambi 62′