Queens yapata ushindi wa jioni dhidi ya Ceasiaa

Bao pekee la dakika ya 90 lililofungwa na Jentrix Shikangwa limetosha kuipa Simba Queens ushindi 1-0 dhidi ya Ceasiaa Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) uliopigwa Uwanja wa KMC Complex.

Shikangwa alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Asha Djafari.

Katika mchezo huo Ceasiaa Queens walicheza kwa nidhamu kubwa ya kujilinda ili wakiipa nafasi Queens ya kumiliki zaidi mchezo.

Kocha Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Aisha Mnuka, Precious Christopher na Elizabeth Wambui na kuwaingiza Asha Djafar, Amina Bilal na Ritticia Nabbosa.

Ushindi huu unaifanya Queens kufikisha alama 34 tukiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 12.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER