Simba yaichakaza bila huruma Yanga Bunge Bonanza

Timu ya Wabunge mashabiki wa Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi mabao 4-0 dhidi ya mashabiki wa Yanga katika Bunge Bonanza likilofanyika katika Uwanja wa Shule ya Sekondari John Merin jijini Dodoma.

Katika mchezo huo Simba ilimiliki sehemu kubwa ambapo ilikuwa na uwezo wa kupata mabao mengi zaidi.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba waliocheza mechi hiyo ambapo aliingia dakika ya 80.

Bonanza hilo lilianza na matembezi pamoja na mbio zilizoanzia Chuo cha Mipango yakiongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, Rais wa TFF, Wallace Karia pamoja na Wabunge na Viongozi mbalimbali wa Serikali.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER