Sare ya kufungana bao tuliyopata ugenini dhidi ya Bravos Do Marquis katika mchezo wa tano wa hatua ya makundi umetufanya kufuzu moja kwa moja hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Abednigo Mosiatlhaga aliwapatia wenyeji bao la mapema dakika ya 13 kufuatia mlinzi wa kati Che Fondoh Malone kurudisha pasi fupi ambayo iliunganishwa na mfungaji huyo.
Baada ya bao hilo tuliongeza kasi ya mashambulizi ili kutafuta bao la kusawazisha ingawa ufanisi wetu mbele ya lango la Bravos haukuwa mzuri.
Leonel Ateba alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 68 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Shomari Kapombe.
Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi 10 tukiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A huku tukisalia na mechi moja.
X1: Odah, Aderito, Teodor, Paciencia (Victor 85′) Rosa, Ferreira, Epalanga (Emmanuel 75′), Matoco (Domingos 65′), Mosiatlhaga (Angelo 65′), Bengue (Celio Zua 75′) Goncalves
Walioonyeshwa kadi: Edmilson 74′
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr, Che Malone, Hamza, Kagoma (Fernandez 45′), Kibu (Okajepha 77′), Ngoma, Ateba (Mashaka 88′), Ahoua (Chamou 88′), Mpanzu (Chasambi 52′)
Walioonyeshwa kadi: Fernandez 79′ Camara 85′