Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Novemba 11 nchini Angola kuikabili Bravos Do Marquis katika mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha Fadlu Davids hakufanya mabadiliko yoyote ukilinganisha na kikosi kilichoanza wiki iliyopita katika ushindi wa bao moja dhidi ya CS Sfaxien.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Abdulrazack Hamza (14), Che Fondoh Malone (20), Yusuph Kagoma (21), Kibu Denis (38), Fabrice Ngoma (6), Leonel Ateba (13), Jean Charles Ahoua (10), Elie Mpanzu (34).
Wachezaji wa Akiba
Ally Salim (1), Karaboue Chamou (2), Augustine Okajepha (25), Mzamiru Yassin (19), Debora Fernandes (17), Ladaki Chasambi (36), Awesu Awesu (23), Edwin Balua (37), Valentino Mashaka (27).