Timu yafanya mazoezi Novemba 11

Kikosi chetu kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Novemba 11 tayari kwa mchezo watano wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravos Do Marquis utakaopigwa Jumapili.

Kikosi kilitakiwa kufanya mazoezi hayo kesho kwenye uwanja huo kwa mujibu wa kanuni lakini imeshindikana kutokana na muda huo kuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wachezaji wote 22 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na wapo kamili kuipigania timu kupata pointi tatu.

Kesho kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho kujiweka sawa kabla ya Jumapili saa moja usiku kwa saa Tanzania kushuka katika Uwanja wa Novemba 11 kuikabili Bravos.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER