Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu Ahmed Ally amesema kikosi chetu leo jioni kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Novemba 11 hapa Angola na sio kesho ambayo ndio inapaswa kikanuni.
Ahmed amesema kesho Uwanja wa Novemba 11 utakuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa hivyo sisi tumepewa ruhusa ya kuutumia leo ili kufidia siku ya kesho.
Tazama video hii hadi mwisho Ahmed amezungumzia hali ya kikosi na ratiba nzima tangu tulivyofika jana mchana.