Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Singida Black Stars

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Liti mkoani Singida kuikabili Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Kocha Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji watano ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi iliyopita dhidi ya JKT Tanzania.

Fadlu amewaanzisha Mohamed Hussein, Yusuph Kagoma, Kibu Denis, Steven Mukwala na Jean Charles Ahoua kuchukua nafasi za Valentine Nouma, Debora Fernandes, Awesu Awesu, Leonel Ateba na Ladaki Chasambi.

Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:

Moussa Camara (26), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Abdurazack Hamza (14), Che Malone Fondoh (20), Yusuph Kagoma (21) Denis Kibu (38), Fabrice Ngoma (6), Steven Mukwala (11), Elie Mpanzu (34), Jean Charles Ahoua (10)

Wachezaji wa Akiba:

Ally Salim (1), Kelvin Kijili (33), Karaboue Chamou (2), Mzamiru Yassin (19), Ladaki Chasambi (36), Debora Fernandes (17), Leonel Ateba (13), Valentino Mashaka (27), Awesu Awesu (23). Alexander Erasto (42).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER