Kocha Mkuu Fadlu Davids ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Black Stars utakuwa mgumu lakini tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunafanya vizuri.
Kocha Fadlu amesema kikosi chetu kipo kwenye hali nzuri na tumepata siku mbili kwa ajili ya mazoezi tangu tulivyocheza mechi ya mwisho dhidi JKT Tanzania.
Fadlu ameongeza kuwa pamoja na ubora walionao Singida lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho kuhakikisha tunashinda mechi.
“Tupo kwenye hatua za mwisho za maandalizi ya mchezo wetu wa kesho, leo jioni tutafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Liti tayari kwa mchezo wa kesho,” amesema Fadlu.
Akizungumzia kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu amesema kila mmoja anafahamu umuhimu wa mchezo wa kesho na yupo tayari kupambana ili timu kupata ushindi.
“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kupambana hadi mwisho kuhakikisha tunapata matokeo ya alama tatu ugenini,” amesema Fadlu.