Matola: Tunaiheshimu JKT Tanzania

Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania utakuwa mgumu na tutaingia uwanjani kwa kuwaheshimu.

Matola amesema JKT haijapata matokeo mazuri katika siku za karibuni lakini bado haiondoi ubora walionao hasa ukizingatia kikosi chao kinaundwa na wachezaji wengi wazoefu.

Matola ameongeza kuwa tutaendelea kufanya mabadiliko ya kikosi mara kwa mara kutokana na ratiba kuwa ngumu hasa ukizingatia tunacheza kila baada ya siku mbili.

“Utakuwa mchezo mgumu lakini tumejipanga na tupo tayari kuhakikisha tunapata pointi tatu nyumbani. Mipango yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi,” amesema Matola.

Kuhusu kuruhusu mabao kwenye kikosi chetu, Matola amesema “kiukweli hilo suala linatuumiza kichwa sana lakini tunalifanyia kazi mazoezini tukianza na mchezo wa kesho.”

Kwa upande wake nahodha wa timu Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wachezaji wapo tayari kupambana kuhakikisha ushindi unapatikana.

“Kikubwa tunahitaji mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kutupa sapoti tunaamini tutapata ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER