Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa katika dimba la Kaitaba mkoani Kagera.
Shomari Kapombe alitupatia bao la kwanza dakika ya 13 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na nahodha Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’.
Kiungo mshambuliaji Awesu Awesu alishindwa kuendelea na mchezo na kufanyiwa mabadiliko baada ya kuumia dakika ya 42 nafasi yake ikachukuliwa na Ladaki Chasambi.
Jean Charles Ahoua alitupatia bao la pili dakika ya 44 kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi nje ya 18 na mlinzi Abdallah Mfuko.
Fabrice Ngoma alitupatia bao la tatu kwa kichwa dakika ya 54 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na Ladaki Chasambi.
Steve Mukwala alitupatia bao safi la nne dakika ya 68 baada ya kumalizia kazi kubwa iliyofanywa na Chasambi ambaye alitoka na mpira kuanzia katikati ya uwanja.
Datius Peter aliipatia Kagera bao la kwanza dakika ya 79 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu na kupiga shuti la chini chini lilomshinda mlinda mlango, Moussa Camara.
Mukwala alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tano dakika ya 84 akimalizia pasi safi kutoka kwa Chasambi.
Kiungo Cleophace Mkandala aliipatia Kagera bao la pili Kwa shuti kali la chini chini dakika ya mwisho ya nyongeza lililomshinda mlinda mlango Camara.
Ushindi huu umetufanya kufikisha alama 34 baada ya kucheza mechi 13 tukirejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.
X1: Chalamanda, Datus, Luhende, Mfuko, Mwijage (Onditi 63′), Seif, Mussa, Feka (Mafie 63′) Manyasi (Mahundi 45′), Shamte, Lwasa (Kiakala 63′)
Walioonyeshwa kadi: Shamte 53′
X1: Camara, Kapombe (Kijili 70′), Zimbwe Jr, Chamou, Hamza, Ngoma (Kagoma 58′), Ahoua, Fernandes (Mzamiru 70′), Mukwala, Mpanzu (Mutale 58′) Awesu (Chasambi 42′)
Walioonyeshwa kadi: