Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Fadlu Davids amefanya mabadiliko ya wachezaji watano ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi iliyopita dhidi ya CS Sfaxien katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha Fadlu amewaanzisha Kelvin Kijili, Valentine Nouma, Karabou Chamou, Mzamiru Yassin na Ladaki Chasambi wakichukua nafasi za Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Abdulrazack Hamza, Deborah Fernandez na Jean Charles Ahoua.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (26), Kelvin Kijili (33), Valentine Nouma (29), Karaboue Chamou (2), Che Malone (20), Mzamiru Yassin (19), Ladaki Chasambi (36), Fabrice Ngoma (6), Leonel Ateba (13), Awesu Awesu (23), Kibu Denis (38).
Wachezaji wa Akiba
Ally Salim (1), Abdulrazack Hamza (14), Mohamed Hussein (15), Yusuph Kagoma (21), Augustine Okajepha (25), Joshua Mutale (7), Jean Charles Ahoua (10), Steven Mukwala (11), Valentino Mashaka (27), Alexander Erasto (42).