Tupo tayari kuikabili Ken Gold Leo

Leo saa 10 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa KMC Complex kuikabili Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Ken Gold haina mwenendo mzuri kwenye Ligi kwa sasa hivyo inatafuta sehemu ya kuamkia hivyo tutakuwa makini kuhakikisha tunapata ushindi katika Uwanja wa nyumbani.

Malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi ingawa tunajua utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia wapinzani wetu Ken Gold wanataka kujinasua kutoka katika nafasi waliyopo.

Fadlu: Nimeifuatilia Ken Gold katika baadhi ya mechi

Kocha Mkuu Fadlu Davids amesema ameifuatilia Ken Gold katika mechi kadhaa na amegundua ni timu bora licha ya changamoto ya kupata matokeo çhanya.

Fadlu amesema katika mchezo dhidi ya Namungo aliiwafuatilia akagundua wanacheza vizuri hivyo tunapaswa kuwa makini.

“Itakuwa mechi ngumu lakini tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda. Kikosi chetu kipo kwenye hali nzuri,” amesema Fadlu.

Awesu: Kila mechi kwetu ni fainali

Kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu amesema kila mechi ambayo tunacheza inakuwa ngumu iwe nyumbani au ugenini hivyo wachezaji wapo tayari kupambana kuhakikisha tunapata ushindi.

Awesu ameongeza kuwa kila timu inahokutana na Simba inapambana zaidi ya uwezo wake ili kupata ushindi ndio maana mechi zetu zimekuwa kama fainali.

“Kila mchezo ambao Simba inacheza ni kama fainali tunajua itakuwa mechi ngumu lakini wachezaji tupo tayari kupambana kuhakikisha ushindi unapatikana,” amesema Awesu.

Hatujawahi kukutana na Ken Gold

Ken Gold ni timu mpya imepanda daraja msimu huu hivyo hatujawahi kukutana katika mechi za mashindano hivyo leo itakuwa mechi ya kwanza.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER