Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kwa ajili ya mchezo wetu Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ken Gold utakaopigwa kesho saa 10 jioni.
Mchezo huo ambao tunategemea utakuwa mgumu kutokana na ubora walionao wapinzani wetu Ken Gold utapigwa katika Uwanja wetu wa nyumbani wa KMC Complex.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu au majeraha ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.