Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema kikosi chetu kipo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wetu wa tatu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien kutoka Tunisia utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili Disemba 15.
Ahmed amesema wapinzani wetu tayari wamewasili huku pia Makamishna wa mchezo wakitarajia kuingia kuanzia Leo.
Tazama mahojiano haya hadi mwisho Ahmed ametoa maelekezo ya jinsi ya kununua tiketi pamoja takwimu zake mpaka sasa.