Simba Queens ipo tayari kuikabili JKT Kesho

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Yussif Basigi amesema kikosi chake kipo kwenye hali nzuri kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya JKT Queens utakaopigwa saa 10 jioni katika Uwanja wa KMC Complex.

Basigi amesema JKT ni timu bora na pia ni miongoni mwa wanaoshindania ubingwa hivyo kupata ushindi dhidi yake ni njia ya kuipunguza nguvu na kujiweka kwenye nafasi nzuri.

Basigi ameongeza kuwa pamoja na ubora walionao JKT lakini hana presha kwakuwa anakiamini kikosi chake na kimepata maandalizi mazuri.

“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, wachezaji wangu wote wapo kwenye hali nzuri. Tunakutana na timu ambayo tupo nayo kwenye mbio za ubingwa kwa vyovyote haiwezi kuwa mechi rahisi lakini tumejipanga,” amesema Kocha Basigi.

Kwa upande wake mchezaji mwandamizi, Asha Rashid ‘Mwalala’ amesema timu ipo tayari kuhakikisha ushindi unapatikana licha ya ugumu wa timu tutakayokutana nayo.

“Sisi wachezaji tupo tayari kufuata maelekezo tutayopewa na walimu wetu, kwetu kila mechi tunaipa umuhimu sawa na kipaumbele chetu ni pointi tatu kwenye kila mchezo,” amesema Mwalala.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER