Tumepoteza dhidi ya CS Constantine

Mchezo wetu wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constantine kutoka Algeria uliopigwa Uwanja wa Chahid Hamlaoui umemalizika kwa kupoteza kwa mabao 2-1.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida huku timu zote zikishambuliana kwa zamu huku mbinu zikiwa zimetawala na zote zikifika mara kadhaa langoni mwa mpinzani.

Nahodha Mohamed Hussein alitupatia bao la kwanza dakika ya 24 baada ya kupiga mpira wa krosi uliotinga wavuni moja kwa moja baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jean Charles Ahoua.

CS Constantine walisawazisha bao hilo dakika ya 47 baada ya mlinzi Abdulrazack Hamza kujifunga katika jitihada za kuokoa mpira wa kona uliounganishwa kwa kichwa na Zakaria Bechaa.

Ibrahim Dibi aliwapatia wenyeji bao la ushindi dakika ya 50 kufuatia walinzi wetu kuchelewa kuondoa hatari.

Baada ya mabao hayo ya haraka timu ilirejea kwenye umakini mkubwa huku tukitengeneza nafasi kadhaa lakini Constantine walikuwa imara kutudhibiti huku wakiwa wengi kwenye eneo lao.

X1: Boussouf, Bellaouel, Benchaira, Baouche, Benchaa (Enow 88′) Dibi, Meddahi, Tahar (Mouki 79′), Merbah, Kaibou (Dadi 79′), Boudrama

Walioonyeshwa kadi: Benchaa 81′

X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 76′), Che Malone, Hamza (Fernandez 55′), Chamou, Ngoma, Kibu, Okajepha (Balua 82′), Ateba (Mukwala 76′), Ahoua

Walioonyeshwa kadi:

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER