Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Chahid Hamlaoui kuikabili CS Constantine kutoka Algeria katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kocha Fadlu Davids Leo amekuja kivingine ambapo amewapanga mabeki watatu wa kati kwa ajili ya kuzuia na kuanzisha mashambulizi.
Kocha Fadlu amewaanzisha kwa pamoja Che Fondoh Malone, Abdulrazack Hamza na Karaboue Chamou.
Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:
Moussa Camara (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Karaboue Chamou (2), Che Malone Fondoh (20), Abdurazak Hamza (14), Augustine Okejepha (25), Fabrice Ngoma (6), Leonel Ateba (13), Jean Charles Ahoua (10), Kibu Denis (38).
Wachezaji wa Akiba:
Ally Salim (1), Kelvin Kijili (33), Valentine Nouma (29), Mzamiru Yassin (19), Deborah Fernandez (17), Awesu Awesu (23), Ladaki Chasambi (36), Edwin Balua (37), Steven Mukwala (11).