Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Chahid Hamlaoui tayari kwa mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constantine utakaopigwa saa moja usiku kwa saa za Tanzania.
Wachezaji wote 22 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na hakuna aliyepata maumivu wala changamoto ya kiafya ambayo itamfanya kuukosa mchezo wa kesho.
Pamoja na hali ya hewa kuwa baridi kali tofauti na ilivyo nyumbani wachezaji wetu wameahidi watapambana hadi mwisho kuhakikisha ushindi unapatikana bila kujalisha changamoto iliyopo.