Tumeanza kwa ushindi Kombe la Shirikisho Afrika

Kikosi chetu kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao moja dhidi ya Bravo Do Marquis kutoka Angola katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tulianza mchezo kwa kasi huku tukifika zaidi langoni mwa Bravo lakini hatukuwa na ufanisi wa kuzitumia vizuri nafasi tulizopata.

Jean Charles Ahoua alitupatia bao hilo pekee dakika ya 26 kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi mmoja wa Bravo kuunawa mpira ndani ya 18.

Mlinda mlango, Moussa alidaka mkwaju wa penati uliopigwa na Emmanuel Edmond dakika ya 47 kufuatia Kibu Denis kumchezea madhambi mchezaji wa Bravo.

Kipindi cha pili tulipunguza kasi na kuwafanya Bravo kufika zaidi langoni kwetu tofauti na dakika 45 za mwanzo ambazo muda mrefu walikuwa wanazuia.

X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr, Hamza, Che Malone, Ngoma, Chasambi (Mzamiru 87′), Okajepha (Fernandez 60′), Mukwala (Ateba 74′) Ahoua (Balua 74′), Kibu (Mutale 60′)

Walioonyeshwa kadi:

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER