Timu yaanza mazoezi kujiandaa na Constantine

Kikosi chetu leo kimeanza mazoezi rasmi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constantine ya Algeria utakaopigwa, Disemba 8.

Baada ya ushindi wa bao moja tuliopata dhidi ya Bravo FC kutoka Angola siku ya Jumatano wachezaji walipewa mapumziko mafupi kabla ya leo kurejea mazoezini kuendelea na maandalizi.

Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo yaliyofanyika katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena na kuongozwa na Kocha Mkuu Fadlu Davids na wasaidizi wake.

Kikosi chetu kinatarajiwa kuondoka nchini Jumatano ya Disemba 4 kikiwa na wachezaji 24 tayari kwa mtanange huo.

Mchezo wetu dhidi ya Constantine utapigwa katika Uwanja wa Chahid Hamlaoui saa 11 jioni nchini Algeria ambapo hapa nyumbani itakuwa saa moja usiku.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER