Leo tumezindua rasmi jezi mpya ambazo tutazitumia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo tutaanza kuzitumia kuanzia Novemba 27.
Hafla ya Uzinduzi wa jezi hizo imefanyika katika Duka kubwa la mzabuni Sandaland The Only One lililopo Kinondoni Dar es Salaam.
Kama ilivyo ada jezi nyekundu itakuwa kwa mechi za nyumbani, nyeupe kwa mechi za ugenini na bluu bahari ikiwa jezi namba tatu.
Tayari jezi zimeanza kuuzwa katika maduka yote ya Sandaland kwa bei ya Shilingi 50,000 nchi nzima.
Jezi za msimu huu zimezingatia ubora kutokana na utengenezaji wake ili kuwafanya Wanasimba kufurahi kila wanapovaa.
Uongozi wa klabu una wasisitiza Wanasimba kuhakikisha wananunua jezi hizo mapema ili Novemba 27 katika mchezo wetu wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bravo kutoka Angola kila mmoja awe nayo.