Timu yetu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefuzu fainali za Afrika (AFCON) baada ya kuibuka na ushindi wa bao dhidi ya Guinea katika mchezo wa mwisho uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Nyota wetu Aishi Manula, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ na Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wa Stars walipambana kwa dakika zote 90 kuhakikisha Tanzania inafuzu hatua hiyo.
Kibu Denis yeye aliingia dakika 45 za kipindi cha pili na alipambana muda wote kuhakikisha anachangia furaha ya Watanzania.
Mlinda mlango wetu Moussa Camara yeye alikuwa upande wa Guinea huku akijitahidi kuokoa michomo kadhaa ya nyota wa Stars lakini hata hivyo bahati haikuwa upande wake.
Taifa Stars imemaliza ya pili kwenye kundi H ikiwa na alama 10 nyuma ya vinara DR Congo yenye pointi 12.
Hii inakuwa mara ya nne Tanzania kushiriki michuano ya AFCON ambapo tulifanya hivyo mwaka 1980, 2019, 2023 na mwakani 2025.