Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ceasiaa Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa Uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali huku tukimiliki sehemu kubwa ya mchezo ambapo tulipata bao la kwanza dakika ya 15 Jentrix Shikangwa ambaye aliwazidi ujanja walinzi wa Ceasiaa.
Mlinzi wa kushoto Dotto Evarist alitupatia bao la pili dakika ya 35 baada ya kupiga mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja.
Shikangwa alitupatia bao la tatu dakika ya 53 baada ya kona fupi ambayo Asha Djafar alimuanzishia Doto ambaye alimtengea tena Asha akapiga krosi ambayo aliiunganisha kwa kichwa.
Asha Rashid ‘Mwalala’ ambaye aliingia kipindi cha pili alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne na kutuhakikishia ushindi ugenini.
Kocha wa Simba Queens Yussif Basigi alifanya mabadiliko ya kumtoa Shelda Boniface na kumuingiza Mwalala.
Ushindi huu unatufanya kufikisha pointi tisa tukiwa juu ya msimamo wa Ligi baada ya kucheza mechi tatu.