Kauli ya Kocha Fadlu kuelekea mchezo dhidi ya KMC

Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakuwa mgumu kutokana na kukutana na timu bora.

Kocha, Fadlu amesema KMC wana kikosi bora pamoja na kocha wao lakini tumejiandaa vizuri kuwakabili na kuondoka na pointi zote tatu.

Kocha Fadlu ameongeza kuwa kikosi kipo kwenye hali nzuri na kimepata siku nne za maandalizi kuelekea mchezo wa kesho ambao utaanza saa 10 jioni katika Uwanja wa KMC Complex.

Akizungumzia hali ya kikosi kocha Fadlu amesema kiungo mshambuliaji Joshua Mutale alipata maumivu katika mchezo dhidi ya Mashujaa lakini itategemea na vipimo vya daktari kama atakuwa sehemu ya kikosi cha kesho.

“Mutale alipata maumivu lakini anaendelea vizuri, Abdulrazack Hamza ameanza mazoezi ingawa hayupo tayari kwa mchezo wa kesho, Yusuph Kagoma na Valentino Mashaka wao bado ni majeruhi,” amesema Kocha Fadlu.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Awesu Awesu amewaita mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kesho ili kuwapa sapoti ambayo itamsaidia kupatikana kwa pointi tatu.

“Mashabiki ni wachezaji wa 12 tunawahitaji sana kwenye mchezo wa kesho nasi tumejipanga kuhakikisha tunawapa furaha,” amesema Awesu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER