Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma kwa ajili ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa FC utakaopigwa Uwanja wa Lake Tanganyika saa 10 jioni.
Wachezaji wote tuliosafiri nao wamefanya mazoezi ya mwisho na wapo tayari kwa mchezo wa kesho.
Katika mazoezi hayo ambayo yameongozwa na Kocha Mkuu Fadlu Davids hakuna mchezaji aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa kesho.
Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi katika Uwanja wa ugenini.