Mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania umeahirishwa

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuahirishwa kwa mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania ambao ulipangwa kuchezwa kesho katika Uwanja wa KMC Complex saa 10:15 jioni.

Afisa Habari wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda amesema sababu ya kuahirishwa kwa mechi hiyo ni baada ya wapinzani wetu JKT Tanzania kupata ajali jana wakiwa njiani kutoka Dodoma kurudi Dar es Salaam.

Boimanda amesema gari lililokuwa limebeba timu ya JKT lilipata ajali wakati wa kurejea jijini Dar es Salaam na kusababisha baadhi ya wachezaji wao kuumia.

“Bodi ya Ligi imepokea taarifa ya kupata ajali wa basi lililokuwa limebeba wachezaji wa timu ya JKT Tanzania iliyosababisha wachezaji kadhaa kupata maumivu na tumethibitisha ambayo yanawafanya kutokuwa timamu kwa ajili ya mchezo wa kesho namba 79 dhidi ya Simba,” amesema Boimanda.

Wakati tukisubiri kupangwa kwa tarehe mpya ya kuchezwa kwa mchezo huo kikosi kitaendelea na maandalizi ya mechi inayofuata dhidi ya Mashujaa itayopigwa Novemba Mosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER